Gavana Waiguru ajiunga na UDA

Muhtasari

• Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru amejiunga na UD Abaada ya kukutana na Naibu Rais William Ruto katika makazi yake rasmi mtaani Karen, Nairobi.

Gavana wa Kirinyaga Anne Mumbi
Gavana wa Kirinyaga Anne Mumbi
Image: MAKTABA

Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru amejiunga na chama cha UDA baada ya kukutana na Naibu Rais William Ruto katika makazi yake rasmi mtaani Karen, Nairobi.

Waiguru ambaye kwa sasa anafanya mkutano wa faragha na Ruto aliandamana na wakilishi wadi kutoka kaunti ya Kirinyaga. Siku chache zilizopita gavana huyo alikuwa amedokeza kwamba angeachana na kambi ya Rais Uhuru Kenyatta na kujiunga rasmi na mrengo wa naibu rais maarufu kama "Hustler nation".

Mwezi mmoja uliopita Waiguru ambaye kwa wakati mmoja alikuwa waziri wa ugatuzi na ambaye amekuwa na uhusiano chachu na Ruto alisema "atasikiliza na kufanya mashauriano ya kina" na wapiga kura kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 2022.

"Siwezi kujaribu kuwa mjinga na kwenda kinyume na watu wangu. Siwezi kujipigia kura, nasikiliza wanataka nini. Je, wanataka nigombee ugavana kwa muhula wa pili?” aliuliza.