Makali ya corona:Jumla ya idadi ya waliopokea chanjo ya corona imefika 5,084,297

Muhtasari
  • Kati ya maambukizi hayo 98 ni wakenya huku 1 akiwa raia wa kigeni,61 ni wanaume huku 38 wakiwa wanawake
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 252,938 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 2.0%
Image: HISANI

Watu 99 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 74,895 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 98 ni wakenya huku 1 akiwa raia wa kigeni,61 ni wanaume huku 38 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 252,938 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 2.0%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,687,142.

Aidha watu 115 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 246,505,77 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 38  wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Watu 3 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona huku jumla idadi ya walioaga dunia ikifika 5,266.

Kuna wagonjwa 481 ambao wamelazwa hospitalini, 1,296 wamejitenga nyumbani.

Huku hayo yakijiri kuna wagonjwa 24 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).