Hofu Ruai baada ya mwili wa mwanamke kupatikana ukiwa umetupwa ndani ya choo

Muhtasari

•Polisi walitoa mwili huo baada ya kupokea ripoti kutoka kwa mtunzaji wa nyumba ambaye alikuwa amepokea malalamishi kutoka kwa wapangaji kuhusu harufu mbaya iliyokuwa inatoka kwa choo.

•Mwili huo ulikuwa umekatakatwa vipande na kuwekwa ndani ya gunia kisha kutupwa ndani ya choo cha shimo.

crime scene
crime scene

Mwili wa mwanamke uliokuwa unaoza ulipatikana ukiwa umetupwa kwa choo katika eneo la Kamulu kaunti ya Nairobi.

Mwili huo ulikuwa umekatakatwa vipande na kuwekwa ndani ya gunia kisha kutupwa ndani ya choo cha shimo.

Polisi walitoa mwili huo baada ya kupokea ripoti kutoka kwa mtunzaji wa nyumba ambaye alikuwa amepokea malalamishi kutoka kwa wapangaji kuhusu harufu mbaya iliyokuwa inatoka kwa choo.

Polisi walipofika kwenye eneo la tukio waliweza kutoa mwili ule ambao tayari ulikuwa umeanza kuoza kuashiria kwamba  ulikuwa umekaa pale kwa muda.

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika mochari huku uchunguzi ukianzishwa ili kutambulisha mwanamke huyo na kubaini kilichosababisha mauaji yake.

Familia ambazo zimekosa mmoja wao hivi karibuni zimehimizwa kutembelea kituo cha polisi cha Kamulu ili kumtambulisha..

Uchunguzi wa maiti umepangwa kufanywa ili kumtambua mwanamke huyo na kusaidia mwili wake kufikia jamaa zake.