Polisi watibua njama za kuteketeza shule Ruai

Muhtasari

• Ulinzi zaidi umewekwa katika shule hiyo kufuatia ripoti kwamba baadhi ya wanafunzi walipanga kuteketeza majengo hayo kwa sababu zisizojulikana.

• Zaidi ya shule 30 zimeteketezwa kwa muda wa mwezi mmoja uliopita hali ambayo inawashangaza wengi.

Bweni la shule la upili ya wasichana ya buruburu lateketea
Image: Hisani

Polisi na wasimamizi wa shule ya upili ya Ruai kaunti ya Nairobi walitibua jaribio la kuteketeza bweni moja usiku wa kuamkia Jumanne.

Ulinzi zaidi umewekwa katika shule hiyo kufuatia ripoti kwamba baadhi ya wanafunzi walipanga kuteketeza majengo hayo kwa sababu zisizojulikana.

Polisi wametoa wito kwa wasimamizi wa shule mbalimbali kuwa waangalifu na kuwafahamisha endapo watashuku njama yoyote ya kuharibu mali za shule.

 Zaidi ya shule 30 zimeteketezwa kwa muda wa mwezi mmoja uliopita hali ambayo inawashangaza wengi.

Kwingineko,

Dereva wa kaunti ya Lamu amelazwa hospitalini baada ya lori alilokuwa akiendesha kukanyaga kilipuzi na kumjeruhi siku ya Jumatatu.

Dereva huyo alikuwa akielekea eneo la Kiunga, Mararani na Sankuri wakati lori lake lilipopita kwenye kilipuzi cha kujitengenezea.

Kilipuzi hicho kinaaminika kuwekwa barabarani na wanamgambo wa al-shabaab ambao bado wanaendesha shughuli zao katika eneo hilo.

Dereva huyo alikimbizwa hospitalini huku watu wengine wawili aliokuwa nao wakiponea bila majeraha.

Maafisa wa usalama wameimarisha msako kuwaondoa wanamgambo wote katika eneo hilo.