Siasa za Kwale, Naibu gavana ataeua mgombea mwenza

Muhtasari

• Achani, ambaye amekua naibu wa gavana Salim Mvurya kuanzia mwaka wa 2013, anataka kurithi kiti hicho kwa tiketi ya chama cha UDA, kinachohusishwa na naibu wa rais William Ruto.

• Naibu gavana aliahidi kuendeleza ushirikiano na Kombo, ili kuendeleza maendeleo yaliyoanzishwa na gavana mvurya

 

Mwakilishi wodi wa Samburu Chirema Kombo, Gavana wa Kwale Salim Mvurya na naibu wa gavana Fatma Achani katika makao makuu ya Kwale siku ya Jumatano
Mwakilishi wodi wa Samburu Chirema Kombo, Gavana wa Kwale Salim Mvurya na naibu wa gavana Fatma Achani katika makao makuu ya Kwale siku ya Jumatano

Naibu gavana wa Kwale Fatma Achani amemtua mwakilishi wodi ya Samburu Josphat Chirema Kombo kuwa mgombea mwenza wake katika kinyang’anyiro cha ugavana wa Kwale mwaka ujao.

Achani, ambaye amekua naibu wa gavana Salim Mvurya kuanzia mwaka wa 2013, anataka kurithi kiti hicho kwa tiketi ya chama cha UDA, kinachohusishwa na naibu wa rais William Ruto.

Siku ya Jumatano, gavana Mvurya aliita kikao cha faragha kuzungumzia swala hilo la mgombea mwenza. Walioudhuria kikao hicho ni pamoja na wazee kutoka eneo la Kinango, Matunga, Lunga Lunga na Mswambweni.

Katika kikao hicho, waliamua kwa kauli moja kumteua Kombo kuwa mgombea mwenza wa Achani.

Akizungumza baada ya mkutano huo, Achani alisema atafuata maelekezo ya wazee hao.

“Naheshimu maamuzi ya wazee na viongozi hawa kumteua Kombo kua mgombea wangu mwenza. Mumenihakikishia kua yeye ndio anafaa katika nafasi hio,” alisema Achani.

Naibu gavana aliahidi kuendeleza ushirikiano na Kombo, ili kuendeleza maendeleo yaliyoanzishwa na gavana mvurya.

Image: FACEBOOK DEPUTY GOVERNOR ACHANI

Licha ya kutokua na umaarufu wa kitaifa, Kombo amekua mwakilishi wodi wa Samburu kuanzia mwaka wa 2013 na amewahi kua mwenyekiti was kamati ya bajeti na ili ya uhusiano wa bunge la Kwale.

Kombo aliahidi kufanya kazi kwa karibu na Achani.

Katika gatuzi la Kwale, makabila ya Wadigo, Waduruma na Wakamba ndio yaliyo na idadi kubwa ya watu.

Gavana Mvurya ni Mduruma huku naibu wake Achani ni Mdigo.

Achani amemteua Kombo ambaye ni Mduruma.

Makabila haya mawili ndio yenye usemi mkubwa kwa siasa za Kwale.

Katibu mkuu was Kilimo Hamadi Boga, ambaye pia anawania kiti cha ugavana Kwale, amemtea Katiba mkuu wa Utalii Safina Kwekwe kua mgombea mwenza.

Boga ni Mdigo na Safina ni Mduruma.

Wengine wanaopigania kiti hicho cha ugavana ni pamoja na Chai Lung’azi, Spika wa kauti ya Kwale Sammy Ruwa, aliyekua mbunge wa Matuga Chirau Mwakwere and Gereza Dena.