IEBC kufunga usajili wa wapiga kura licha ya kutoafikia idadi ya wapiga kura wapya waliolengwa

Muhtasari

•Mahakama kuu ya Eldoret kutupilia mbali agizo la kuendeleza shughuli hilo ambalo lilikuwa limetolewa siku ya Jumatatu.

•IEBC imetangaza kwamba shughuli hiyo itafungwa leo (Ijumaa) mwendo wa saa kumi na moja unusu jion

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati

Tume ya uchaguzi na mipaka nchini (IEBC) itakamilisha shughuli ya kusajili wapiga kura jioni ya Ijumaa.

Hii ni baada ya mahakama kuu ya Eldoret kutupilia mbali agizo la kuendeleza shughuli hilo ambalo lilikuwa limetolewa siku ya Jumatatu.

Mpiga kura Patrick Cherono pamoja na wakili wake Kairia Nabasenge walikuwa wamewasilisha kesi mahakamani wakilalamikia kuwa tume ya  IEBC haikuwa imeafikia lengo lake la kusajili wapiga kura wapya milioni 4.5.

Cherono alitaka mahakama kuamuru IEBC kuendeleza shughuli ya usajili wa wapiga kura kwa kipindi cha miezi mitatu zaidi.

IEBC imetangaza kwamba shughuli hiyo itafungwa leo (Ijumaa) mwendo wa saa kumi na moja unusu jioni.

Ripoti ya wapiga kura wapya ambao watakuwa wamesajiliwa kufikia wakati wa kukamilika kwa shughuli hiyo itatolewa punde baada ya kufungwa.

Hapo awali IEBC ilikuwa imedai kwamba haina uwezo wa kuendeleza shughuli ya kusajili wapiga kura ikilalamikia uhaba wa fedha.