Wakenya wasiopiga kura kutozwa faini!

Muhtasari

• Wananchi waliofikisha umri wa kupiga kura lakini hawataki kupiga kura wanafaa kutozwa faini.

• Kulingana na takwimu kutoka Tume ya Uchaguzi na mipaka nchini (IEBC), Kaunti ya  Tana River ilikuwa na jumla ya wapiga kura wapatao 118,327.

Mwanasiasa Maur Bwanamaka akikabidhi mipira kwa timu ya mashinani katika huko ovo, Tana River.
Mwanasiasa Maur Bwanamaka akikabidhi mipira kwa timu ya mashinani katika huko ovo, Tana River.
Image: KNA

          Kulingana na takwimu kutoka Tume ya Uchaguzi na mipaka nchini (IEBC), Kaunti ya  Tana River ilikuwa na jumla ya wapiga kura wapatao 118,327.

           Kwingineko, wakaaji wa Ovo wamewataka viongozi wao hasa gavana kuhakikisha ardhi yote huko Tana River inafanyiwa usoreveya na wamiliki wake kupewa hati miliki. Pia walilamikia uhaba wa chakula na njaa katika eneo hilo, kwani hawajapata mvua kwa muda mrefu sasa.

          Hata hivyo, Kamishna wa Kaunti ya Tana River Mbogai Rioba alisema serikali kuu tayari imezindua zoezi la ugavi wa chakula cha msaada kwa familia zilizoathiriwa na janga la ukame kote nchini.

Wananchi waliofikisha umri wa kupiga kura lakini hawataki kupiga kura wanafaa kutozwa faini.

Mgombea wa kiti cha seneta katika Kaunti ya Tana River Maur Bwanamaka amependekeza kufanyia sheria marekebisho ili kufanya upigaji kura kuwa jambo la lazima kwa kila mwananchi.

           Akizungumza katika hafla ya kuchangia timu ya mpira ya Kijiji cha Ovo, Wadi ya Chewani ili kununua viatu kwa wachezaji wake, Bwanamaka alisema kuwa idadi ndogo ya watu waliojitokeza kujisajili kama wapiga kura imechangiwa na hali ya watu kukata tamaa kutokana na msukumo wa maisha.

         “Inapasa kupitishwa sheria itakayofanya upigaji kura kuwa lazima kwa kila raia anapofikisha miaka 21. Hii itawasaidia Wakenya kuwa na nidhamu na kufanya maamuzi yafaayo ili kuhakikisha viongozi wasiowajibika hawachaguliwi kamwe,’’ alisisitiza Bwanamaka.