Covid-19: Watu 178 wapatikana na corona,31 wapona

Muhtasari
  • Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 84
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,057 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 2.5%
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,750,273
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MAKTABA

Watu 178  wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 7,091 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 173 ni wakenya huku 5 wakiwa ni raia wa kigeni,90 ni wanaume huku  88 wakiwa wanawake.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 84.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,057 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 2.5%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,750,273.

Aidha watu 31 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 247,489,25 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 6 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Hii leo hamna maafa ambayo yamerekodiwa nchini, huku idadi ya walioga dunia ikisalia kuwa 5,314.

Kuna wagonjwa 403 ambao wamelazwa hospitalini, 1,063 wamejitenga nyumbani.

Huku hayo yakijiri kuna wagonjwa 30 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 5,751,332.