Makali ya corona:Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 5,813,553

Muhtasari
  • Mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 4 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 83
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,151 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 2.5%
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,757,038
Image: HISANI

Watu 94  wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 6,765 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 91 ni wakenya huku 3wakiwa ni raia wa kigeni,55 ni wanaume huku  39 wakiwa wanawake.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 4 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 83.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,151 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 2.5%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,757,038.

Aidha watu 38 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 247,527,33 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 5 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Mtu mmoja ameaga dunia kutokana na corona huku idadi jumla ya walioaga dunia ikifika 5,315.

Kuna wagonjwa 405 ambao wamelazwa hospitalini, 1,059 wamejitenga nyumbani.

Huku hayo yakijiri kuna wagonjwa 30 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 5,813,553.