Jamaa amuua mkewe na mamake Moiben

Muhtasari

• Mshukiwa mwenye umri wa miaka 34, Wilfred Kiptoo alimvamia mkewe na kumuua kabla ya kuuchoma mwili katika kijiji cha Sokonini. 

Pingu
Image: Radio Jambo

Polisi mjini Eldoret wamemkamata mwanamume aliyemuua mkewe na mamake usiku wa kuamkia Alhamisi nyumbani kwao katika kaunti ndogo ya Moiben. 

Mshukiwa mwenye umri wa miaka 34, Wilfred Kiptoo alimvamia mkewe na kumuua kabla ya kuuchoma mwili katika kijiji cha Sokonini. 

Kamanda wa polisi wa Uasin Gishu Ayub Gitonga alisema mshukiwa alimgeukia mamake mwenye umri wa miaka 64 na kumpiga na kifaa butu alipojaribu kuingilia kati. 

Watoto wawili waliokuwa ndani ya nyumba hiyo walipiga kamza na majirani waliofika eneo la tukio waliwapata wawili hao tayari wamefariki. 

Gitonga alisema bado wanachunguza sababu za mauaji hayo. Polisi walimwokoa mshukiwa kutoka kwa wanakijiji waliokuwa na hasira na walitaka kumuua. 

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya rufaa ya Moi.