Stress free! Sonko aendelea kula raha licha ya masaibu yake

Muhtasari

Sonko alibanduliwa kutoka kiti cha gavana wa Nairobi na bunge la kaunti mwaka jana na kisha uamuzi huo kuidhinishwa na seneti.

Image: FACEBOOK// MIKE SONKO

Licha ya kupoteza matumaini yote kurejea ofisini kama gavana wa Nairobi, Mike Sonko anaendlea na maisha yake bila stress.

Katika Video aliyotundika kwenye akaunti yake ya Twitter gavana huyo wa zamani wa Nairobi anaonekana akinengua maungo akiwa nyumbani kwake na wageni wake.

Sonko alibanduliwa kutoka kiti cha gavana wa Nairobi na bunge la kaunti mwaka jana na kisha uamuzi huo kuidhinishwa na seneti.

Hakuchoka aliwasilisha kesi mahakamni kupinga kufurushwa kwake lakini siku chache zilizopita mahakama ilitupilia mbali kesi yake na kutoa nafasi ya kuapishwa kwa naibu gavana Anne Kananu kuwa gavana wa Nairobi.

Alikubali uamuzi wa korti.