Muhtasari
•Maafisa wa DCI waliwasilisha ombi la kutaka Mwendwa azuiliwe katika Kituo cha Polisi cha Gigiri.
Polisi wameomba mahakama iwaruhusu wamzuie rais wa shirikisho la soka nchini Nick Mwendwa kwa siku 14 zaidi ili kukamilisha uchunguzi.
Maafisa wa DCI waliwasilisha ombi la kutaka Mwendwa azuiliwe katika Kituo cha Polisi cha Gigiri.
Mwendwa alikamatwa Ijumaa iliyopita kwa madai ya ufisadi.
Alipelekwa katika Makao Makuu ya DCI ambako alihojiwa kuhusu jinsi FKF ilitumia shilingi milioni 430 milioni ambazo FKF ilikabidhiwa kuendesha shughuli za kandanda mnamo mwaka wa 2016
Mwendwa pia alipewa shilingi milioni 44 zilizoongezwa kwa shirikisho kuandaa Harambee Stars kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2019.
Mengi yatafuata....