Milipuko miwili yaripotiwa Kampala Uganda

Muhtasari

Milipuko miwili imetokea katika mji mkuu wa Uganda , Kampala.

Image: KWA HISANI

Milipuko miwili imetokea katika mji mkuu wa Uganda , Kampala.

Ripoti zinaonyesha kuwa mlipuko mmoja ulitokea kwenye jumba la maduka karibu na kituo cha Polisi cha Central na mwingine karibu na Bunge.

Majengo ya ofisi yalitikisika wakati milipuko hiyo ilipoanza, baadhi ya mashahidi wamesema.

Chanzo cha milipuko hiyo, au iwapo kumekuwa na majeruhi, bado haijathibitishwa.

Mwezi uliopita, milipuko miwili tofauti nchini humo iliua watu wawili. Mmoja ulimuua mhudumu katika baa na mwingine, mshambuliaji wa kujitoa mhanga ambaye alikuwa ameingiza vilipuzi kwenye basi.

Mamlaka nchini humo zimeshutumu milipuko hiyo ya Oktoba dhidi ya kundi la waasi wa Kiislamu lenye makao yake makuu nchini Uganda, DR Congo, Allied Democratic Forces.

Takriban watu 50 wamekamatwa, na wengine kushtakiwa mahakamani, tangu matukio hayo ya hivi majuzi.