Usajili wa vijana katika awamu ya tatu ya mpango wa Kazi Mtaani kuanza

Muhtasari

‚ÄĘKatibu Mkuu wa Idara ya Nyumba na Maendeleo ya Mijini Charles Hinga ametangaza kuwa watu wanaotaka kuhudhuria watahitajika kujiandikisha kwenye tovuti ya Mfumo wa Usimamizi wa Kazi Mtaani (KMS).

Kazi mtaani
Kazi mtaani
Image: MAKTABA

Habari na Maureen Kinyajui

Mpango wa kuajiri vijana katika awamu ya tatu ya  mradi wa Kazi Mtaani unaanza siku ya Ijumaa kabla ya kuzinduliwa rasmi mwezi  Desemba.Awamu ya tatu inasemekana kuwa imara na itatekelezwa katika makazi zaidi ya 900 katika kaunti zote 47  za Kenya.

Mradi huo utaendelea hadi mwisho wa Juni 2022 na kupatia riziki maelfu ya vijana ambao watajiunga nao.

Katibu Mkuu wa Idara ya Nyumba na Maendeleo ya Mijini Charles Hinga ametangaza kuwa watu wanaotaka kuhudhuria watahitajika kujiandikisha kwenye tovuti ya Mfumo wa Usimamizi wa Kazi Mtaani (KMS).

KMS ni mfumo wa simu na mtandao uliotengenezwa na Serikali ya Kenya ili kusajili na kusimamiawanufaika wa Kazi Mtaani kote nchini

"Tovuti ya mtandaoni itahakikisha wale wanaotaka wanasajiliwa kwa wakati, uwazi na ufanisi ambao utakuwa sawa," Hinga alisema.

Programu ya wavuti itatumika kusajili, kuchakata data iliyopokelewa kutoka kwa programu ya rununu, malipo na kuripoti.Kwa upande mwingine, programu ya simu ya mkononi itatumika kukusanya wafanyakazi, saa na saa na data ya miradi.

Mwezi uliopita wakati wa Siku ya Mashujaa , rais Uhuru Kenyatta aliahidi kwamba mradi wa kitaifa wa usafi almaarufu kama Kazi Mtaani ungeendelezwa kwa sababu ulikuwa na matokeo chanya katika maisha ya mamia ya maelfu ya vijana.