Wakenya watahitajika kuonyesha thibitisho ya kuchajwa kikamilifu ili kupokea huduma- Wizara ya afya

Serikali zinajadili iwapo zitaweka vizuizi msimu wa sikukuu

Muhtasari

• Wakenya pia watahitajika kuthibitisha wamechajwa kikamilifu wanapotumia huduma za usafiri kama vile SGR, matatu, mabasi na ndege zinazobeba hapa nchini.`

•Waziri wa afya Mutahi Kagwe alisema wananchi watahitajika kuonyesha thibitisho ya kuchajwa ili kuruhusiwa kuingia katika maeneo ya umma kama hifadhi za wanyama, hoteli, baa na hoteli

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe na mwenzake wa Utalii baada ya taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu Covid-19 katika Afya House, Nairobi mnamo Novemba 21.
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe na mwenzake wa Utalii baada ya taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu Covid-19 katika Afya House, Nairobi mnamo Novemba 21.
Image: ANDREW KASUKU

Habari na Magdaline Saya

Wakenya watahitajika kunyesha thibitisho kwamba wamechajwa ili kuweza kupokea huduma mbalimbali za serikali kuanzia Desemba 21, 2021.

Siku ya Jumapili wizara ya afya ilitangaza Wakenya watalazimika kuwa wamechajwa ili kuweza kupokea huduma za KRA, elimu, NTSA, Uhamiaji, huduma za  bandari na kuweza kutembeleana katika hospitali na magereza.

Isitoshe, Wakenya pia watahitajika kuthibitisha wamechajwa kikamilifu wanapotumia huduma za usafiri kama vile SGR, matatu, mabasi na ndege zinazobeba hapa nchini.`

Madereva, kondakta, waendesha bodaboda, marubani na wafanyikazi wengine kwa ndege watahitajika kubeba thibitisho kuwa waamechajwa kila wakati.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe alisema wananchi watahitajika kuonyesha thibitisho ya kuchajwa ili kuruhusiwa kuingia katika maeneo ya umma kama hifadhi za wanyama, hoteli, baa na hoteli.

Mikakati hiyo ambayo ilitangazwa  na wizara ya Afya ili kuongeza upokeaji wa chanjo ya  COVID 19 nchi pia itahitaji wafanyabiashara wote wakiwemo wafanyabiashara wadogo na wa kati wenye zaidi ya watu 50 kwa siku kuweka vibao vinavyohitaji uthibitisho wa chanjo kabla ya kuingia ndani ya jengo hilo.

"Hakuna mtu amesema ni lazima, ikiwa hutaki huduma katika Wizara ya Afya usije. Hakuna mtu anayesema kwamba lazima upewe chanjo, sio kabisa. Ninachosema ni kwamba ikiwa unataka kuja ofisini kwangu na nimechanjwa kikamilifu na hutaki kujaribu simu wakati kila mtu amechanjwa kikamilifu, sio sawa," Kagwe alisema.

Kulingana na mikakati mipya, mikusanyiko yote ya ndani itahitajika kuwa na theluthi mbili ya watu na kila atakayehudhuria kuthibitisha amechajwa. 

Waziri wa utalii Najib Balala alitangaza watalii wote kutoka maeneo ya Ulaya lazima wawe wamechajwa kikamilifu na waonyeshe thibitisho ili waruhusiwe kuingia nchini.

Serikali zinajadili iwapo zitaweka vizuizi msimu wa sikukuu huku mataifa mengine kama Austria yakifunga nchi.