Shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty International tawi la Kenya limetoa wito kwa serikali ya Kenya kutowalazimisha raia wake kupewa chanjo ya Covod -19.
Katika taarifa shirika hilo lilsema: 'Kamati ya kitaifa ya kukabiliana na janga la Corona iharakishe programu za elimu zinazofaa ili kushughulikia chanjo kwa uwazi na kushughulikia taarifa potofu'.
''Ingawa kuna sababu halali za afya ya umma kwa watu wengi iwezekanavyo kupata chanjo, sababu hizi zisiwanyime watu haki ya kufanya kazi, kupata huduma muhimu zikiwemo elimu, afya na usalama pamoja na uhuru wao wa kutembea. Haya yote ni haki za kimsingi na uhuru wa kikatiba,'' ilisema taarifa hiyo.