Covid-19:Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 6,700,134,52 wapona

Muhtasari
  • Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 6,700,134
  • Watu 46 wamepatikana na  maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuli 4,913 chini ya saa 24 zilizopita
  • Kati ya maambukizi hayo wote ni wakenya,31 ni wanaume huku 15 wakiwa wanawake
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MOH

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 6,700,134.

Watu 46 wamepatikana na  maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuli 4,913 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo wote ni wakenya,31 ni wanaume huku 15 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,862 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 0.9%.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 5 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 79.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,816,173.

Vile vile watu 52 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 248,070,30 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 22 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Mtu mmoja ameaga dunia kutokana na corona huku idadi jumla ya walioaga dunia ikifika 5,333.

Kuna wagonjwa 351 ambao wamelazwa hospitalini, 966 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 17 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).