Makali ya corona: Watu 42 wapatikana na corona,15 wapona

Muhtasari
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,904 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 0.8%
  • Mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 13 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 95
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,821,144
Image: HISANI

Watu 42 wamepatikana na  maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuli 4,971 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo  40  ni wakenya huku 2 wakiwa raia wa kigeni,21 ni wanaume huku 21 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,904 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 0.8%.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 13 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 95.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,821,144.

Vile vile watu 15 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 248,085,13 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 2 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Hamna mtu ambaye ameaga dunia kutokana na maambukizi ya covid-19, huku idadi hiyo ikisalia kuwa  5,333.

Kuna wagonjwa 358 ambao wamelazwa hospitalini, 971 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 16 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 6,811,043