Uhuru kuongoza hafla ya kufuzu kwa maafisa wa KDF

Muhtasari

• Jumla ya maafisa 320 watafuzu kwa katika hafla hiyo baada ya kutimiza mafunzo maalum ya kijeshi.  

Rais Uhuru Kenyatta anapokelewa na waziri wa Ulinzi Monica Juma na Mkuu wa mkuu wa majeshi ya KDF Jenerali Robert Kibochi katika Kambi ya Navy, Manda Bay katika Kaunti ya Lamu Septemba 23, 2021. Picha: PSCU

Rais Uhuru Kenyatta leo ameratibiwa kuongoza hafla ya kufuzu kwa maafisa wa KDF wa daraja la Cadet. 

Jumla ya maafisa 320 watafuzu kwa katika hafla hiyo baada ya kutimiza mafunzo maalum ya kijeshi.  

Usalama umeimarishwa katika hafla hiyo ambayo itafanyika kuambatana na kanuni za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Covid-19.  

Rais Kenyatta ambaye amekuwa nje ya nchi tangu Novemba 18 akiwa kwa ziara rasmi nchini Msumbiji, Afrika Kusini na Uganda aliwasili nchini Alhamisi jioni.  

Rais Kenyatta amekuwa akijaribu kutafuta suluhu kwa mzozo wa uongozi nchini Ethiopia unaohusisha serikali ya Kitaifa na wapiganaji wa Tigray.