Makali ya corona:Visa 32 vipya vya corona vimerekodiwa nchini,18 wapona

Muhtasari
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 255,469 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 1.1%
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,858,654
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MOH

Watu 32 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 2,893 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 31 ni wakenya huku 1 akiwa raia wa kigeni,17 ni wanaume huku 15 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 255,469 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 1.1%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,858,654.

Aidha watu 18 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 248,444,15 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 3 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Hakuna mtu ameaga dunia  kutokana na corona huku idadi jumla ya walioaga dunia ikifika 5,335.

Kuna wagonjwa 212 ambao wamelazwa hospitalini, 837 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 4 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 7,583,134.