Mbunge wa zamani wa Mwingi ahusika katika ajali mbaya ya barabarani

Muhtasari

•Mutambu ambaye alipoteza wanafamilia kadhaa katika mkasa huo wa basi alielekea Mwingi baada ya basi hilo kutolewa mtoni.

Mbunge wa zamani wa Mwingi Joe Mutambu
Mbunge wa zamani wa Mwingi Joe Mutambu
Image: MAKTABA

Mbunge wa zamani wa Mwingi ya kati Joe Mutambu alinusurika kifo baada ya kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani  katika barabara kuu ya Thika-Mwingi Jumapili usiku.

Dereva wake alifariki papo hapo kufuatia ajali hiyo iliyohusisha trekta mwendo wa saa tano usiku katika eneo la Kavenge.

Mutambu alikuwa anarejea Nairobi kutoka eneo la Nuu ambapo basi la shule ya sekondari ya St. Joseph Seminary Mwingi lilitumbukia ndani ya mto Enziu na kuua takriban watu 33.

Mutambu ambaye alipoteza wanafamilia kadhaa katika mkasa huo wa basi alielekea Mwingi baada ya basi hilo kutolewa mtoni.

Gari lililohusika katika ajali
Gari lililohusika katika ajali
Image: MUSEMBI NZENGU

Gari lake lilibingirika mara kadhaa baada ya kugongana na trekta.

Mwanasiasa huyo pamoja na abiria wengine ambao walijeruhiwa walikimbizwa katika hospitali ya Matuu Level 4 kupokea matibabu.

Mwili wa dereva ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali hiyo.

(Utafsiri: Samuel Maina)