Covid-19: Watu 75 wapatikana na corona,8 wapona,2 waaga dunia

Muhtasari
  • Visa 75 vipya vya maambukizi ya Covid-19  vimerekodiwa nchini kutoka kwa sampuli 4,771 chini ya saa 24 zilizopita
  • Kati ya maambukizi hayo 60 ni wakenya huku 15 wakiwa raia wa kigeni,50 ni wanaume huku 25 wakiwa wanawake
Image: HISANI

Visa 75 vipya vya maambukizi ya Covid-19  vimerekodiwa nchini kutoka kwa sampuli 4,771 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 60 ni wakenya huku 15 wakiwa raia wa kigeni,50 ni wanaume huku 25 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 255,544 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 1.6%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,863,425.

Aidha watu 8 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 248,452,5 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 3 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Watu 2 ameaga dunia  kutokana na corona huku idadi jumla ya walioaga dunia ikifika 5,337.

Kuna wagonjwa 207 ambao wamelazwa hospitalini, 844 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 2 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 7,678,464.