Mwanafunzi ashtakiwa kwa kujaribu kuteketeza bweni - Mwala

Muhtasari

• Akiwa mbele ya Hakimu Mkazi, Nelly Kenei, mwanafunzi huyo alikanusha Mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya kibinafsi ya Shilingi 10,000.  

• Mshukiwa anadaiwa kwamba akiwa pamoja na wengine ambao hawakuwa mbele ya mahakama walijaribu kuteketza bweni la Kwame Nkurumah usiku wa Novemba 9 na 10.

Pingu
Image: Radio Jambo

Mwanafunzi wa shule ya upili ya Makutano Boys katika kaunti ndogo ya Mwala, siku ya Jumanne alifikishwa katika mahakama ya Wamunyu kwa kujaribu kuchoma bweni la shule.  

Akiwa mbele ya Hakimu Mkazi, Nelly Kenei, mwanafunzi huyo alikanusha Mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya kibinafsi ya Shilingi 10,000.  

Mshukiwa anadaiwa kwamba akiwa pamoja na wengine ambao hawakuwa mbele ya mahakama walijaribu kuteketza bweni la Kwame Nkurumah usiku wa Novemba 9 na 10 majira ya saa sita usiku kinyume na kifungu cha 333(a) cha kanuni za adhabu.  

Mahakama iliamuru Kamati maalum ya kumtetea mwanafunzi huyo iteue wakili ili amwakilishe. Kesi hiyo itasikizwa Aprili 4,2022.   

Katika mahakama hiyo wanaume watatu walihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kila mmoja kwa kosa la kushambulia. Mahakama iliwapata Samuel Nzivo, Stephen Ngumbi na Samuel Nzivo na hatia ya kumpiga na kumdhuru Joseph Muthini, katika eneo la Mango, Kaunti Ndogo ya Mwala mnamo Mei 10, 2019.  

Mahakama iliambiwa watatu hao wakiwa na chuma, fimbo na kisu, walimvamia mlalamishi na kumjeruhi kichwani, kifuani, mgongoni na miguuni.