Uhuru atia saini miswada mitano ya bunge kuwa sheria

Muhtasari
  • Uhuru atia saini miswada mitano ya bunge kuwa sheria
Rais Uhuru Kenyatta
Image: PSCU

Rais Uhuru Kenyatta ametia saini miswada mitano ya bunge kuwa sheria.

Mkuu wa Nchi aliidhinisha Mswada wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Mswada wa Marekebisho ya Mswada wa Benki Kuu ya Kenya na Mahakama ya Rufaa ya Ushuru (Marekebisho).

Pia iliyotiwa saini kuwa sheria ni Mswada wa Wadhamini (Marekebisho) na Mswada wa Bima ya Amana ya Kenya (Marekebisho).

Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi, mwenzake wa Seneti Ken Lusaka, Waziri wa Hazina Ukur Yatani na Mkuu wa Utumishi wa Umma Joseph Kinyua walihudhuria hafla fupi ya kutia saini.

Image: PSCU

Wengine walikuwa Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Amos Kimunya, Wakili Mkuu Ken Ogeto na Naibu Mkuu wa Wafanyakazi Ikulu Njee Muturi.