Raila Odinga kuwania kiti cha urais mwaka ujao

Muhtasari
  • Wakati huo huo kinara huyo amezindua rasmi Azimio la Umoja.

Kinara wa chama cha ODM Raila Amollo Odinga katika kongama la Azimio la Umoja ametangaza kwamba ataania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Pia wakati huo huo alitangaza uzinduzi wa Jumuiya ya Azimio La Umoja ambayo itakuwa gari lake hadi Ikulu.

"Ninakubali kujiwasilisha kama mgombeaji wa Urais kwenye Uchaguzi wa Urais mnamo Agosti 9, 2022 kufuatia ombi na uamuzi wa pamoja wa AZIMIO LA UMOJA," amesema Odinga.

Tangazo lake lilikuwa siri iliyofichwa lakini sasa linamsafishia njia kukabiliana na Naibu Rais William Ruto, ambaye pia bado hajatangaza azma yake lakini pia ni siri iliyofichwa.

“Sigombei urais ili kumpinga yeyote bali kupendekeza sera bora. Niko katika mbio hizi za kufinyanga taifa moja lisilogawanyika. Sina vita na watu binafsi, niko vitani na itikadi ambazo zingeongoza taifa hili katika mwelekeo mbaya,” alisema.

Kongamano la Odinga la Azimio La Umoja lilihudhuriwa na maelfu ya wafuasi wake waliokuwa na hamu wakiongozwa na wanasiasa, wengi ambao walikuwa wapinzani wake wakubwa miaka ya nyuma lakini wamejipanga nyuma yake na kuahidi kumuunga mkono.

Mengi yafuata;