Willy Paul akana madai ya ubakaji

Muhtasari

Kupitia video ambayo Willy Paul aliweka kwa ukurasa wake wa Twitter, alisema Diana Marua anataka kutumia jina lake ili ajulikane.

Image: INSTAGRAM// WILLY PAUL

Msanii sifika Wilson Radido almaarufu Willy Paul amejitokeza wazi wazi na kujitetea dhidi ya  madai yaliyokuwa yakisambaa mtandaoni ya kuwa alimbaka Diana Marua miaka mitatu iliyopita

Kupitia video ambayo Willy Paul aliweka kwa ukurasa wake wa Twitter, alisema Diana Marua anataka kutumia jina lake ili ajulikane.

“Najua watu hawataniamini ,lakini yote Diana alisema kunihusu mmi kumbaka ni uongo mtupu. Sijawahi baka mtu mimi, ambia bwana yako ukweli”  Pozee alisema

Aliendelea  kusema kuwa siku Diana alilala kwake  ilikuwa kwa hali yake na ilikuwa makubaliano baina yao wawili. Hivyo akamuomba  Diana amweleze bwanake nini kilifanya aende kwake

Diana hivi karibuni amesikika akisema Pozee alimvuta kwa gari  na kumpeleka kwake, jambo ambalo lilimfanya ajifanye mgonjwa lakini Willy Paul hukumsikiza.

Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Kutokana na habari hizo ndio maana msanii huyo kajitokeza wazi na kujitetea akisema kwamba kilichotendeka yalikuwa makubaliano baina yao wawili.

Ikimbukwe hivi karibuni  Pozee alizua madai kwamba Bahati ameninunulia Diana marua ‘views’ kwa Youtube na kumuomba aache kumuingiza kwa mamabo yake.

“Diana, unajua mambo yetu tafadhali kuwa na tahadhari kwa mambo unayosema baina yetu. Kwa sababu bwana yako anakununulia views pale youtube usione kama tunatoshana, wewe bishana na Queen P. Tuachie hapo kwa sasa” Willy Paul alisema.