•Le General ni mwanamuziki mwenye aliyekuwa na kipaji cha kutunga na kuimba nyimbo kwa sauti nyororo na yakuvutia kwa wapenzi wa Rhumba.
Mwanamuziki nguli wa nyimbo za Rhumba kutoka Congo, Le General Defao Matumona amefariki dunia nchini Cameroon .
Defao ambaye alikuwa na umri wa takriban miaka 62 amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi. Kifo chake kimejiri wakati akiwa ziarani ya kuwatumbuiza mashabiki wake nchi ya Cameroon.
Mwanamuziki huyo alizaliwa Disemba 03, 1958, Kinshasa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Le General ni mwanamuziki aliyekuwa na kipaji cha kutunga na kuimba nyimbo kwa sauti nyororo na yakuvutia kwa wapenzi wa Rhumba. Alijizolea umaarufu mkubwa kwa miondoko yake ya Ndobolo.
Aliweza kutambulika rasmi kwenye tasnia ya muziki wa Rhumba mnamo mwaka wa 1976, wakati alitoa nyimbo kubwa kama School of love, Kikuta family na Sidewalk
Wanamuziki Fally Ipupa na Ferre Gola walikuwa miongono mwa wa kwanza kuwasilisha ujumbe wao wa rambirambi, wakieleza kifo chake kuwa ni hasara kwa Afrika