Ruto ashinda raundi ya kwanza bungeni katika kura ya muswada wa miungano

Muhtasari

•Wabunge wanaogemea upande wa  Ruto walifanikiwa kupata  wabunge 123 wa kuyapigia kura marekebisho hayo dhidi ya 118  kutoka upande wa Uhuru Kenyatta.

Bunge la Kenya
Bunge la Kenya
Image: Twitter @NAssembly Kenya

Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga wapata pigo baada ya wabunge wanaogemea upande wa Naibu rais, William Ruto kushinda awamu ya kwanza katika azma yao kutupilia mbali muswada wa marekebisho katika vyama vya kisiasa.

Wabunge wanaogemea upande wa  Ruto walifanikiwa kupata  wabunge 123 wa kuyapigia kura marekebisho hayo dhidi ya 118  kutoka upande wa Uhuru Kenyatta.

Muswada huo ambao unaruhusu kuundwa kwa vyama vya muungano umepata pigo baada ya wabunge wa mrengo wa Ruto kuwazidi wenzao ambao walikuwa wameleta muswada huo.

Kufuatia ushindi huo  Bunge limeruhusu marekebisho yaliyopendekezwa na Mbunge wa Tigania Magharibi, John Mutunga.

Wabunge wa Ruto wamepanga marekebisho ili kupunguza nguvu muswada huo uliobakisha hatua moja kuwa sheria 

 Wabunge wanaomuunga mkono kinara wa ODM na Rais Uhuru Kenyatta wanataka muswada huo upitishwe bila marekebisho yeyote

Wabunge wa Tangatanga wamepanga marekebisho pamoja na mengine kudhoofisha ofisi ya Msajili wa Vyama .

Kulingana na wabunge wanaomuunga mkono Ruto, Mswada uliopendekezwa na Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Amos Kimunya unaipa afisi ya Anne Nderitu mamlaka ya kifalme