Covid-19:Watu 1,223 wapatikana na corona,2,436 wapona,10 waaga dunia

Muhtasari
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 299,732 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 30.6%
  • Mgonjwa wa chini ana umri wa miezi 7 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 101
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,046,316
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MAKTABA

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 1,223 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 nchini kutoka kwa sampuli 4,003 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 1,132 ni wakenya huku 576 wakiwa raia wa kigeni,91 ni wanaume huku 647 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 299,732 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 30.6%.

Mgonjwa wa chini ana umri wa miezi 7 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 101.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,046,316.

Vile vile watu 2,436 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 256,551,2,335 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 101 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Watu 10 wameaga dunia kutokana na corona huku idadi ya walioaga ikifika 5,394.

Kuna wagonjwa 1,089 ambao wamelazwa hospitalini, 24,349 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 50 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 10,134,012.