Covid-19:Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 10,310,606,2,216 wapatikana na corona

Muhtasari
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 304,350 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 25.6%
  • Mgonjwa wa chini ana umri wa miezi 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 105
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,065,623
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MOH

Watu 2,216 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 nchini kutoka kwa sampuli 8,669 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 1,984 ni wakenya huku 232 wakiwa raia wa kigeni,1,124 ni wanaume huku 1,092 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 304,350 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 25.6%.

Mgonjwa wa chini ana umri wa miezi 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 105.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,065,623.

Vile vile watu 775 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 259,308, 578 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 197 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Kwa habari za kuhuzunisha Watu 3 wameaga dunia kutokana na corona huku idadi ya walioaga ikifika 5,404.

Kuna wagonjwa 1,226 ambao wamelazwa hospitalini, 25,969 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 51 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 10,310,606