Mbwembwe katika hafla ya siku ya kuzaliwa ya Raila

Muhtasari

• Bomas of Kenya ilipambwa kwa rangi zote nyeupe, bluu na chungwa katika kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Raila.

• Kundi la Warembo na Baba lilikuwa limevalia fulana za bluu na maneno yaliyoandikwa kwa rangi nyeupe.

Kiongozi wa ODM Raila Odinga baada ya kupata kipande cha keki katika ukumbi wa Bomas of Kenya kwa sherehe za miaka 77 ya kuzaliwa kwake. Picha: FREDRICK OMONDI
Kiongozi wa ODM Raila Odinga baada ya kupata kipande cha keki katika ukumbi wa Bomas of Kenya kwa sherehe za miaka 77 ya kuzaliwa kwake. Picha: FREDRICK OMONDI

Kiongozi wa ODM Raila Odinga amewasili katika ukumbi wa Bomas of Kenya kwa sherehe za miaka 77 ya kuzaliwa kwake.

Hafla hiyo inaenda sambamba na uzinduzi wa Azimio la Young Turks.

Waziri Mkuu huyo wa zamani alifika ukumbi wa Bomas akiandamana na mkewe Ida mwendo wa saa 11.30 alfajiri pamoja na viongozi mbalimbali.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria ni Gavana wa Nairobi Anne Kananu, kakake Raila, Oburu Odinga, Katibu Mkuu wa ODM Edwin Sifuna, na wabunge wengi wakiwemo Babu Owino (Embakasi Mashariki), Anthony Oluoch (Mathare Kaskazini), Esther Passaris (Mwakilishi wa Wanawake wa Nairobi).

Siku ya kuzaliwa ya Raila Odinga huko Bomas of Kenya. Picha/ Fredrick Omondi
Siku ya kuzaliwa ya Raila Odinga huko Bomas of Kenya. Picha/ Fredrick Omondi

Katibu Tawala Mkuu Wizara ya Michezo, Utamaduni na Urithi ndiye Mgeni Rasmi.

Bomas of Kenya ilipambwa kwa rangi zote nyeupe, bluu na chungwa katika kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Raila.

Mavazi ni mchanganyiko wa rangi tatu au mguso wa yoyote kati yao.

Kundi la Warembo na Baba lilikuwa limevalia fulana za bluu na maneno yaliyoandikwa kwa rangi nyeupe.

Wanawake pia walivaa kofia za bluu zenye maandishi sawa.

Warembo na Baba kutoka Mombasa Chapter waliongeza kitambaa cha chungwa kwenye vazi lao.

Hafla za kuadhimisha kuzaliwa kwa Raila pia ziliandaliwa katika maeneo mbali ya nchi katika kaunti za Nyeri, Nakuru, Mombasa na nyinginezo.

Mwakilishi wa wanawake wa Mombasa Aisha Hussein akiwa na mwanasiasa wa Mombasa Beatrice Gambo, Mbunge wa Mvita Abulswamad Nassir na mwanasiasa Mohamed Soud Machele wakikata keki kusherehekea miaka 77 ya kuzaliwa kwa kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga iliyoadhimishwa katika eneo la Tudor kaunti ya Mombasa siku ya Ijumaa. Picha / John Chesoli

Keki ya siku ya kuzaliwa pia imepambwa kwa rangi tatu.

Wanaume pia hawakusazwa walitawala hafla hiyo wakiwa na kofia za rangi ya chungwa huku Azimio Young Turks wakiwa wamevalia fulana za bluu.