"Nilikimbiwa nikaachwa na mimba" Nyota Ndogo azungumzia maisha yake

Muhtasari

•Nyota Ndogo alieleza changamoto alizokumbana nazo alipoachwa na mpenzi  wake akiwa mjamzito .

Nyota Ndogo na mwanawe
Nyota Ndogo na mwanawe
Image: Hisani

Mwanamuziki  Nyota Ndogo Alhamisi alisimulia masaibu aliyopitia wakati akiwa na mimba. 

Kupitia ukurasa wake wa Facebook alieleza taabu alizokumbana nazo wakati aliachwa na mpenzi  wake baada ya kumtunga mimba.

"Tumetoka mbali. Nakumbuka nikizuiliwa hospitali kwa kukosa pesa kulipia gharama za kujifungua. Nilikaa hospitalini wiki moja hatukua na pesa. sikuona marafiki hata kuja kunitembelea" Nyota alieleza 

Aliendelea kuelezea maisha yalivyomwendea kombo akiwa mjamzito kwa mwanake wa pili.

"Nikipata ujauzito wa pili nilikuwa single nyie hata mimi nilikimbiwa nikaachwa na mimba yangu lakini nilijipanga niliweka pesa nyingi  yaani nikazaa na operesheni niwe sawa bila kuomba nilitaka kuonja hospitali  kubwa kwa hivyo nilijilipia Hospitali ya Mombasa" Alisema. 

Nyota Ndogo ambaye anatambulika sana kwa kibao Kuna watu na Viatu  alisema aliyoyapitia maishani yamekuwa funzo kwake na kumfanya kulea familia yake bila kutegemea mtu yeyote 

"Jamani ukiumwa na nyoka utaogopa nyasi tu. Mungu mkubwa. Ndio huwa sipendi unafiki binadamu nawajua sana. watakuchekesha ukiwa sawa. ukikosa hawakujui. bora hata nyinyi mashabiki"