Makali ya corona:Watu 3,611 wapona corona huku asilimia ya maambukizi ikifika 20.8%

Muhtasari
  • Visa 1,034 vipya vya maambukizi ya corona vimerekodiwa nchini kutoka kwa sampuli 4,975 chini ya saa 24 zilizopita
  • Kati ya maambukizi hayo 851 ni wakenya huku 183 wakiwa raia wa kigeni,504 ni wanaume huku 530 wakiwa wanawake
Image: HISANI

Visa 1,034 vipya vya maambukizi ya corona vimerekodiwa nchini kutoka kwa sampuli 4,975 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 851 ni wakenya huku 183 wakiwa raia wa kigeni,504 ni wanaume huku 530 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 312,572 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 20.8%.

Mgonjwa wa chini ana umri wa miezi 5 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 103.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,104,457.

Vile vile watu 3,611 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 268,573, 3,493 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 118 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Kwa habari za kuhuzunisha Watu 8 wameaga dunia kutokana na corona huku idadi ya walioaga ikifika 5,454.

Kuna wagonjwa 1,225 ambao wamelazwa hospitalini, 23,107 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 45 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 10,609,955.