Raila ni tajiri lakini ni mchoyo - Ruto

Muhtasari

Alisema Raila anamiliki kampuni za mabilioni ya pesa lakini hawezi kuwasaidia wasiojiweza na maskini.

Ruto alisema Kenya iko tayari kwa kiongozi ambaye ana nia ya kuhakikisha kuwa kuna fursa sawa kwa raia wake wote bila kujali hali zao za kijamii.

Raila mara kadhaa ametilia shaka chanzo cha utajiri wa Ruto huku akihoji vile anatoa mamilioni ya pesa kama misaada kwa makundi tofauti wakati wa kampeni zake.

Ruto (kushoto) na Odinga (kulia), walikuwa 'maswahiba' wanaotarajia kusigana katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2022
Ruto (kushoto) na Odinga (kulia), walikuwa 'maswahiba' wanaotarajia kusigana katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2022
Image: GOOGLE

Naibu rais William Ruto mwishoni mwa wiki alimsuta kiongozi wa ODM Raila Odinga kwa kukashifu wema wake wa kufadhili makundi mbali mbali na mazoea yake ya kutoa pesa.

"Kwa nini wanahangaika na mimi kutoa Shilingi 2 milioni; hizo ni pesa kidogo sana ambazo wanazo lakini ni wa choyo sana," Ruto alisema.

Alisema Raila anamiliki kampuni za mabilioni ya pesa lakini hawezi kuwasaidia wasiojiweza na maskini.

Raila mara kadhaa ametilia shaka chanzo cha utajiri wa Ruto huku akihoji vile anatoa mamilioni ya pesa kama misaada kwa makundi tofauti wakati wa kampeni zake.

Wakati huo huo, Ruto aliwataka wakazi wa Magharibi mwa Kenya kuunga mkono azma yake ya urais.

Alizungumza katika soko la Ekitale huko Kanduyi, kaunti ya Bungoma.

Alisema amejitolea kubadilisha maisha ya Wakenya wa kawaida.

Ruto alisema Kenya iko tayari kwa kiongozi ambaye ana nia ya kuhakikisha kuwa kuna fursa sawa kwa raia wake wote bila kujali hali zao za kijamii.

Aliahidi kupunguza gharama ya uzalishaji wa kilimo iwapo atachaguliwa kuwa rais.

Ruto alisema gharama ya sasa ya uzalishaji zinamnyanyasi mkulima.

“Tutahakikisha kuwa tunapunguza gharama ya ukulima ili wakulima wadogo wafurahie jasho la ukulima wao,” Ruto alisema.