Wahamiaji haramu 91 kutoka Ethiopia watiwa mbaroni Kitengela

Muhtasari

•91 hao  ambao wote ni wanaume walikamatwa baada ya kuvunja nyumba moja ya kibinafsi waliyokuwa wamewekwa katika mtaa wa Milimani ulio eneo la Kitengela, kaunti ya Kajiado.

Pingu
Image: Radio Jambo

Wahamiaji haramu 91 wenye asili ya Ethiopia wanazuiliwa katika vituo vya polisi vya Milimani na Kitengela baada ya kukamatwa siku ya Jumapili.

91 hao  ambao wote ni wanaume walikamatwa baada ya kuvunja nyumba moja ya kibinafsi waliyokuwa wamewekwa katika mtaa wa Milimani ulio eneo la Kitengela, kaunti ya Kajiado.

Uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kwamba wahamiaji hao (44 kati yao ambao ni wadogo) waliingizwa nchini kwa trela na walikuwa wanashikiliwa kwa muda huku wasafirishaji haramu wakitafuta njia za kuwasafirisha hadi nchi nyingine.

Kitengo cha DCI kinaendelea na uchunguzi kuhusiana na kisa hicho kufuatia ongezeko la wahamiaji haramu hapa nchini ile kudhoofisha shughuli za usafirishaji haramu wa binadamu na kuwakamata wahusika.

Wahamiaji haramu waliokamatwa Jumapili wanatarajiwa kuhojiwa na na kufanyiwa taratibu nyingine za kisheria.

Wahamiaji hao walionekana wachovu na wenye njaa huku baadhi yao wakiwa nusu uchi.