Covid-19:Watu 1,105 wapatikana na corona,3,320 wapona,8 waaga dunia

Muhtasari
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 313,677 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 15.9%
  • Mgonjwa wa chini ana umri wa mwezi 1 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 102
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,111,402
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MAKTABA

Visa 1,105 vipya vya maambukizi ya corona vimerekodiwa nchini kutoka kwa sampuli 6,945 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 1,051 ni wakenya huku 54 wakiwa raia wa kigeni,534 ni wanaume huku 571 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 313,677 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 15.9%.

Mgonjwa wa chini ana umri wa mwezi 1 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 102.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,111,402.

Vile vile watu 3,320 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 271,893, 2,991 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 329 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Kwa habari za kuhuzunisha Watu 8 wameaga dunia kutokana na corona huku idadi ya walioaga ikifika 5,462.

Kuna wagonjwa 1,223 ambao wamelazwa hospitalini, 21,411 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 42 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 10,696,021.