Richard Onyoka akamatwa na Makachero wa DCI

Muhtasari

•Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji kuelekeza Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai kuchunguza madai ya chuki katika matamshi yake.

Richard Onyonka
Richard Onyonka
Image: twitter/ Richard Onyonka

Mbunge wa Kitutu Chache Kusini Richard Onyoka amekatwa na Kikosi cha Makachero wa DCI, katika kaunti ya  Kisii.

Richard Onyoka  amekamatwa Jumanne asubuhi baada ya agizo la Mkurugenzi wa Mashtaka Noordin Haji kumuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai kuchunguza madai ya chuki katika matamshi yake.

Kulingana na barua ya DPP na kanda ya video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii  Onyoka anaonekana akihutubia  wakazi huku akionekana kutumia maneno yanayodaiwa kueneza chuki. 

Inarejelea kanda ya video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo Mhe Richard Onyoka, mbunge wa Kitutu Chache anahutubia mkutano katika Kaunti ya Kisii.

Matamshi yanayodaiwa kunaswa kwenye kwenye video huenda ni kunyume na Kifungu 33(2) cha Katiba ya Kenya 2010.