Covid-19: Watu 4,126 wamepona corona,813 wapatikana na corona,7 waaga dunia

Muhtasari
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 314,490 kiwango cha maambukizi cha asilimia 13.5%
  • Mgonjwa wa chini ana umri wa miezi 4 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 103
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,117,407
Image: HISANI

Visa 813 vipya vya maambukizi ya corona vimerekodiwa nchini kutoka kwa sampuli 6,005 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 656 ni wakenya huku 157 wakiwa raia wa kigeni,421 ni wanaume huku 392 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 314,490 kiwango cha maambukizi cha asilimia 13.5%.

Mgonjwa wa chini ana umri wa miezi 4 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 103.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,117,407.

Vile vile watu 4,126 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 271,893, 3,968 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 158 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Kwa habari za kuhuzunisha Watu 7 wameaga dunia kutokana na corona huku idadi ya walioaga ikifika 5,469.

Kuna wagonjwa 1,201  ambao wamelazwa hospitalini, 17,443 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 47 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).