Magaidi hawa wanane hatari wanasakwa na DCI

Muhtasari

• DCI imesema washukiwa hao wametumwa hapa nchini ili kutekeleza mashambulizi ya kigaidi. 

Image: TWITTER// DCI

Kitengo cha upelelezi wa Jinai (DCI) kimetoa ombi kwa Wakenya kujitolea kwa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa washukiwa wanane wa ugaidi wanaohusishwa na Alshabaab.

Kupitia kwa tangazo lililochapishwa Jumatano, DCI imesema washukiwa hao wametumwa hapa nchini ili kutekeleza mashambulizi ya kigaidi. 

DCI imechapisha sura za washukiwa hao pamoja na maelezo yatakayosaidia wananchi kuwatambua.

Mohammed Ali Hussein:

Image: DCI

-Mmoja wa wanamgambo wa Alshabaab waliopanga kufanya shambulizi lililozuiliwa Somalia mnamo 2018.

Ahmed Ali Mohammed

-Mmoja wa wanamgambo wa Alshabaab waliopanga kufanya shambulizi lililozuiliwa Somalia mnamo 2018.

Abdurahman Hija aka  Mnubi

-Mzaliwa wa kaunti ya Nyeri.

- Mmoja wa genge lililohangaisha wakazi wa Nyeri kabla ya kutorokea Somalia.

-Alijiunga na Alshabaab 2016. 

-Alitumwa nchini kutekeleza mashambulizi baada ya kupewa mafunzo ya kigaidi.

Image: DCI

Erick Njoroge Wachira/ Mohammed Njoroge/ Moha

-Alizaliwa mnamo Agosti 27, 1991 katika kaunti ya Nyeri.

-Alikuwa mmoja wa genge ambalo lilihangaisha wakazi wa eneo la Mukurweini na Karatina.

- Alijiunga na Alshabaab 2016.

Image: dci

Abdikadir Mohammed Abdikadir/ Ikrima

-Mzaliwa wa eneo la Ukasha, Somalia. 

-Anahusishwa na kikundi cha Al-Qaeda nchini Yemen

-Alihusika katika kupanga shambulizi la Dusit mnamo 2019 na lingine la Kampala mnamo 2010.

-Aliwahi kuishi South C, Kongowea na Mombasa.

Image: DCI

Peter Gichungu Njoroge almaarufu kama Mustafa 

-Mzaliwa wa Kiambaa, kaunti ya Kiambu mnamo 1988.

-Alihitimu na Bachelor of Science Degree in Informatio Technology katika chuo kikuu cha JKUAT. 

-Alikamatwa mjini Mandera mnamo Julai 6, 2016 akielekea Somalia.

-Baadae alitorokea Somalia na kujiunga na Alshabaab pamoja na mpenzi wake Miriam Hamisi kutoka Bamburi, Mombasa.

Image: dci

Mohamud Abdi Aden/ Mohammed Yare/ Ibrahim/ Mohamed Hassan/ Mohamud Abdirahman

-Ametoka kaunti ya Garissa.

-Alikamatwa mara ya kwanza 2014 kwa kupatia Alshabaab taarifa za maeneo ya kushambulia nchini Kenya.

-Mmoja wa waliopanga shambulizi la Dusit mnamo 2019.

Image: DCI

Kassim Musa Mwarusi/ Abu Miki

-Ametoka eneo la Ukunda.

-Alikuwa mmoja wa genge lililohangaisha wakazi wa Pwani Kusini.

-Anaaminika kuzulu maeneo ya Likoni, Diani na Ukunda mara kwa mara.

Image: DCI