Mudavadi asusia mkutano wa vinara wa OKA Elementaita

Muhtasari

• Mudavadi hajahudhuria mkutano muhimu mjini Naivasha unaotarajiwa kuafikiana kuhusu mpeperushaji bendera ya urais wa muungano wa Oka. 

• Kutokuwepo kwa Musalia katika mkutano wa huo muhimu kumetia shaka kujitolea kwake kwa muungano huo (Oka) na kunaweza kuashiria kuporomoka kwa muungano huo. 

• Vinara wengine Kalonzo Musyoka(Wiper), Moses Wetangula(Ford Kenya) na Gideon Moi wa Kanu kwa sasa wako Elmentaita.

 Kinara wa chama cha Amani National Congress Musalia Mudavadi hajahudhuria mkutano muhimu mjini Naivasha unaotarajiwa kuafikiana kuhusu mpeperushaji bendera ya urais wa muungano wa Oka. 

Kutokuwepo kwa Musalia katika mkutano wa huo muhimu kumetia shaka kujitolea kwake kwa muungano huo (Oka) na kunaweza kuashiria kuporomoka kwa muungano huo. 

Vinara wengine Kalonzo Musyoka(Wiper), Moses Wetangula(Ford Kenya) na Gideon Moi wa Kanu kwa sasa wako Elmentaita (Nakuru) ambapo wanakutana na kamati ya kiufundi ya Oka kujadiliana kuhusu mapendekezo ya taratibu za kumteua mgombea wa muungano huo. 

Hii ni licha ya habari kuchipuka siku ya Ijumaa asubuhi kwamba kamati ya kiufundi ilikuwa imeafikiana kwamba Kalonzo ndiye kinara bora kupeperusha bendera ya Oka. 

Siku ya Ijumaa na wakati mkutano wa vinara wengine ukiendelea, Musalia alitumia akaunti yake ya Tweeter kutangaza kwamba 'dhoruba yaja ('storm is coming.').'

 "A storm is coming! Who can you trust,(Dhoruba inakuja! Nani unaweza kumwamini)," Musalia aliandika kwenye twitter akiwataka Wakenya wakutane naye katika ukumbi wa Bomas of Kenya. 

Alifuata hii kwa hashtag  #Tusidanganye#KenyaKwanza. Matamshi hayo yalizua uvumi kwamba Musalia anaweza kuwa anarejelea usaliti fulani ndani ya muungano wa Oka. 

Chama cha ANC cha Musalia kinatazamiwa kufanya Kongamano la Wajumbe wa Kitaifa Januari 23 ili kumuidhinisha kama mgombea urais wa chama hicho Agosti 9.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO