•Nick Ruto amefunga pingu za maisha na mpenzi wake wa miaka mingi Evelyn Chemtai katika hafla ya kitamaduni inayojulikana kama koito miongoni mwa jamii ya Wakalenjin.
Mwanawe naibu rais William Ruto, Nick Ruto amefunga pingu za maisha na mpenzi wake wa miaka mingi Evelyn Chemtai katika hafla ya kitamaduni inayojulikana kama koito miongoni mwa jamii ya Wakalenjin.
Nick ambaye ni mtoto wa kwanza wa Ruto alipiga hatua hiyo muhimu maishani mnamo Jumamosi Januari 15, 2022 katika kiwanja cha Windy Ridge Karen.
Haya yanajiri takriban miezi sita baada ya bintiye naibu rais, June Ruto kufunga ndoa na mpenzi wake Alexander Ezenagu kutoka Nigeria.
Nick Ruto ni wakili na tayari ameonyesha nia ya kuijiunga na siasa siku zijazo akifuata nyayo za baba yake ambaye anatazamia kuridhi rais Uhuru Kenyatta.