Mshtuko baada ya Afisa kupatikana amefariki katika lango la kituo cha polisi cha Kimende

Muhtasari

•Afisa huyo hakufika katika kituo cha polisi cha Kimende wala katika makao makuu ya kaunti ndogo ya Lari ambako alikuwa anafanya kazi.

Wakaazi wa Kimende katika kaunti ndogo ya Lari wakitazama mwili wa afisa wa polisi aliyefariki Ijumaa.
Wakaazi wa Kimende katika kaunti ndogo ya Lari wakitazama mwili wa afisa wa polisi aliyefariki Ijumaa.
Image: GEORGE MUGO

Polisi walisema marehemu alikuwa katika likizo baada ya kuugua na alikuwa anaelekea nyumbani.

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Lari Stephen Kirui alisema afisa huyo alikuwa anafanya kazi katika kituo cha polisi cha Taveta kilicho katika kaunti ndogo ya Taveta.

Kirui alisema kwa kuwa afisa huyo alikuwa katika likizo aliamua kwenda kupumzika nyumbani kwao Baringo.

"Likizo ya wagonjwa ilitiwa saini wiki jana Jumatano katika kituo cha polisi cha Taveta na hivyo akaondoka," Kirui alisema.

"Kwa kuwa alihudumu katika eneo la Kimende miaka miwili iliyopita, aliamua kushuka kutoka kwa gari alilokuwa akisafiria huko Kimende ili kuwaangalia baadhi ya maafisa ambao walikuwa marafiki zake," akaongeza.

Wakaazi wa mji wa Kimende katika kaunti ndogo ya Lari wakitazama mwili wa afisa wa polisi aliyefariki Ijumaa.
Wakaazi wa mji wa Kimende katika kaunti ndogo ya Lari wakitazama mwili wa afisa wa polisi aliyefariki Ijumaa.
Image: GEORGE MUGO

Hata hivyo, afisa huyo hakufika katika kituo cha polisi cha Kimende wala katika makao makuu ya kaunti ndogo ya Lari ambako alikuwa ametumwa, Kirui alisema.

"Tunashuku kuwa alizidiwa nguvu na ugonjwa wake na kuanguka kando ya barabara ya lango la posta na kufa."

"Tunachunguza kisa hicho ili kubaini kilichosababisha kifo chake. Mwili wake ulikuwa mzima bila majeraha. Mali zake ambazo zilikuwa kwenye begi pia zilipatikana bila kuguswa," Kirui aliongeza.

Tukio hilo lilivutia umati mkubwa wa watu ambao walishuku kuwa ni mkazi aliyeuawa na mwili wake kuletwa mahali hapo na wauaji.

(Utafsiri: Samuel Maina)