Makali ya corona:16 wapoteza maisha yao,762 wapatikana na corona

Muhtasari
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 319,011 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 9.8%
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,164,789
Waziri wa afya Mutahi Kagwe
Image: Wilfre Nyangaresi

Siku ya Jumatano waziri wa afya Mutahi Kagwe alithibisha kwamba watu 762 walipatikana na wamepatikana na maambukizi ya corona nchini kutoka kwa sampuli 7,780 chini ya saa 24 zilizopita.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 319,011 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 9.8%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,164,789.

Vile vile watu 657 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 287,140, 532 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 125 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Maafa ya corona imezidi kupanda na idadi hiyo kufikia 5,520 baada ya watu 16 kuaga dunia kutokana na corona.

MUtahi alisema kuwa Kuna wagonjwa 915 ambao wamelazwa hospitalini, 8,493 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 45 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 11,259,226.