Covid-19:Watu 1,123 wapona corona,300 wapatikana na corona

Muhtasari
  • Visa 300 vya  maambukizi ya corona vimerekodiwa nchini kutoka kwa sampuli 6,072 chini ya saa 24 zilizopita
  • Kati ya maambukizi hayo 274 ni wakenya huku 26 wakiwa raia wa kigeni,158 ni wanaume huku 142 wakiwa wanawake
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 320,138 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 4.9%
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe akutana na Baraza la Magavana mjini Mombasa mnamo Desemba 15.
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe akutana na Baraza la Magavana mjini Mombasa mnamo Desemba 15.
Image: MAGDALINE SAYA

Visa 300 vya  maambukizi ya corona vimerekodiwa nchini kutoka kwa sampuli 6,072 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 274 ni wakenya huku 26 wakiwa raia wa kigeni,158 ni wanaume huku 142 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 320,138 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 4.9%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,183,057.

Vile vile watu 1,123 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 289,547, 1,001 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 122 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Watu 3 wameaga dunia kutokana na maambukizi ya corona huku idadi hiyo ikifika 5,531.

Kuna wagonjwa 814 ambao wamelazwa hospitalini, 6,801wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 46 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 11,522,950.