Mkenya wa kwanza kutangaza hali yake ya HIV aaga dunia

Dkt Muriuki ameishi na virusi vya Ukimwi kwa kipindi cha zaidi ya miaka 30.

Muhtasari

•Muriuki alisita kumeza madawa ya ARV kwa kipindi cha miaka 27 akidai kwamba alidhibiti hali yake kwa kula liche bora, kufanya kazi na kuwa na mtazamo mzuri wa maisha.

•Alikuwa miongoni mwa Wakenya wa kwanza kunywa dawa ya Kemron ambayo ilitengenezwa na watafiti wa Kenya.

Raia wa kwanza wa Kenya kutangaza wazi kwamba anaugua ugonjwa wa UKIMWI, Joe Muriuki ameaga dunia.

Kifo cha Muriuki kimethibitishwa na shirika la Nephak ambalo husaidia watu wanaoishi na VVU hapa nchini.

Dkt Muriuki ameishi na virusi vya Ukimwi kwa kipindi cha zaidi ya miaka 30.

Muriuki alisita kumeza madawa ya ARV kwa kipindi cha miaka 27 akidai kwamba alidhibiti hali yake kwa kula liche bora, kufanya kazi na kuwa na mtazamo mzuri wa maisha.

Marehemu alitangaza kwamba ameathiriwa na VVU mnamo mwaka wa 1987, akiwa Mkenya wa kwanza kupiga hatua hiyo.

Alikuwa miongoni mwa Wakenya wa kwanza kunywa dawa ya Kemron ambayo ilitengenezwa na watafiti wa Kenya.

Muriuki alihudumu katika mahakama ya VVU kama mwakilishi wa watu wanaoishi na VVU na alikuwa mwanachama wa jopo kazi la kikanda lililofanya kazi katika uundaji wa sheria ya kusimamia VVU ya Afrika Mashariki.

Mnamo mwaka wa 2017 Muriuki aliomba kuteuliwa katika Bunge la Afrika Mashariki ili kuwakilisha watu wanaoishi na UKIMWI.