Mabasi ya shule yanayofanya kazi baada ya 6:30 jioni yakamatwe- Magoha

Muhtasari

• Waziri wa elimu George Magoha amewaonya walimu wakuu dhidi ya kurusu mabasi ya shule kuondoka shuleni baada ya 6:30 jioni.

• Kwa upande wake waziri wa usalama wa kitaifa, Fred Matiang’i ameunga mkono hatua hiyo huku akisema kwamba safari za usiku ni hatari kwa wanafunzi.

Waziri wa Elimu George Magoha
Waziri wa Elimu George Magoha
Image: MAKTABA

Waziri wa elimu George Magoha amewaonya walimu wakuu dhidi ya kurusu mabasi ya shule kuondoka shuleni baada ya 6:30 jioni.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi funguo na kufuli za konteina za kuhifadhi karatasi za mitihani ya kitaifa kwa wakurugenzi wa kaunti, Magoha alisema kwamba wakuu wa shule ambao watakwenda kinyume na amri hiyo watachukuliwa hatua za kisheria.

“Nawaomba maafisa wote wa zamu kuyakamata mabasi yote ambayo yatakuwa barabarani baada ya saa kumi na mbili jioni,” Magoha alisema.

Kwa upande wake waziri wa usalama wa kitaifa, Fred Matiang’i ameunga mkono hatua hiyo huku akisema kwamba safari za usiku ni hatari kwa wanafunzi.

“Tutawakamata wakuu wote wa shule kwa kukiuka amri hiyo. Mabasi ya shule yasiruhiusiwe kufanya safari zozote baada ya 6:30 mjioni,” Matiang’i alisema.

Mawaziri hao wawili walikuwa wanazungumza baada ya shambulio la basi la shule ya upili ya Mogil iliypo kaunti ya Elgeyo Marakwet lililofanyika siku ya Alhamisi. Dereva aliyekuwa akiendesha basi hilo aliuawa pamoja na wanafunzi kumi na watatu huku walimu wawili wakijeruhiwa.

Waziri Matiang’i alisema kwamba mwalimu mkuu wa shule hiyo atakamatwa kwa kukiuka sheria hiyo.

Shambulio hilo lilitokea mnamo saa nne usiku katika barabra ya Arror- Mogil karibu na eneno la Tot katikakaunti ya Elgeyo Marakwet.

Baadhi ya waliojeruhiwa wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Kapsowar huku mwakiwa katika hali mbaya.

Wanafunzi hao pamoja na walimuwakiwa katika msafara wa mabasi matatu ya shule ya Tot, Kerio Valley na shule ya upili ya Mogil.

Mabasi hayo yalishambuliwa ghafla karibu na shule ya msingi ya Chesunan iliyopo  Marakwet magharibi wakati ambapo walikuwa wakirudi katika shule ya upili ya Tot iliypo Marakwet kaskazini.

Magaidi hao waliokuwa wamejihami walishambulia basi la shule ya upili ya Mogil na kumuua dereva, huku wakiwamiminia risasi walimu na wanafunzi waliokuwemo basini humo.