OKA yatangaza kujiunga na muungano wa Azimo la Umoja

Muhtasari
  • OKA yatangaza kujiunga na muungano wa Azimo la Umoja
Wakuu wa OKA wasaini makubaliano na kiongozi wa NARC-Kenya Martha Karua
Image: Andrew Kasuku

Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka ametangaza rasmi kuingia kwake na kwa One Kenya Alliance katika vuguvugu la Azimio La Umoja.

"Muungano wa One Kenya Alliance ungependa kufahamisha Wakenya kwamba umeanzisha rasmi mazungumzo ya wazi na yaliyopangwa yenye itikadi kama hizo - muungano wa Jubilee na chama cha ODM," Kalonzo alisema.

Kiongozi wa Wiper alisema wataunda muungano mkuu na timu ya Azimio ambayo itaitwa Azimio- One Kenya Alliance,

Kalonzo aliongeza kuwa OKA imefikia uamuzi wa kuongeza uungwaji mkono wao Azimio tangu ODM na Jubilee ziangazie itikadi na mipango yake ya kisiasa kwa taifa.

“Kama OKA, tunaamini kwa uthabiti mazungumzo ya wazi, ya uaminifu na yaliyopangwa ambayo msingi wake ni kukuza umoja wa kitaifa; kudumisha na kuheshimu utu wa Wakenya wote; kukomesha utamaduni wa ufisadi na kutokujali, na kurejesha adabu ya kuishi ndani ya mipaka yetu,” alieleza.

Makamu huyo wa zamani wa rais alifichua pia kwamba nyaraka rasmi zingetiwa saini Jumatatu, Februari 28, 2022, na kisha hati ya makubaliano itawasilishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.