Kivutha Kibwana amwambia Kalonzo asilete 'confusion' Azimio

Muhtasari

• Hatimaye gavana wa kaunti ya Makueni, Kivutha Kibwana amezungumzia hatua ya kinara wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka kujiunga na muungano wa Azimio.

• “Sisi hatuna shida Wiper ikija katika Azimio…Lakini wakija wajue wamekuja wakiwa wamechelewa na wakae katikaviti ambavyo  watu waliochelewa hukaa,” Kibwana alisema.

Hatimaye gavana wa kaunti ya Makueni, Kivutha Kibwana amezungumzia hatua ya kinara wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka kujiunga na muungano wa Azimio.

Kibwana amemkashifu  Kalonzo kwa kutofanya maamuzi ya haraka kuhusu msimamo wake mbele ya uchaguzi wa mwezi Agosti, na kumtaka kutotoa mahitaji mengi kabla ya kujiunga na Azimio.

Akizungumza na wakazi wa eneo la Ukambani, Kivutha alisema kwamba yeye pamoja na magavana Charity Ngilu wa Kitui na Alfred Mutua wa Machakos tayari walikuwa wamechukua nafasi yao ndani ya muungano wa Azimio na kwamba wana mchango mkubwa katika kuhakikisha matakwa ya wakazi wa eneo hilo yanasikika na kushughulikiwa.

Kulingana na Kibwana, Kalonzo amejiunga kuchelewa katika muungano wa Azimio, na hivyo hapaswi kivyovyote vile kuwa na imani kubwa kuhusu kupata nafasi kubwa katika kambi hiyo.

 “Sisi hatuna shida Wiper ikija katika Azimio…Lakini wakija wajue wamekuja wakiwa wamechelewa na wakae katikaviti ambavyo  watu waliochelewa hukaa,” Kibwana alisema.

“Lakini kuja kusema kwamba ati sasa wanataka viti vya  mbele, tumefanya kazi, tunaendelea na kazi, hatutaki mchanganyiko."

Ikumbukwe kwamba kulingana na taarifa ya OKA iliyosomwa na Kalnzo Musyoka, muungano huo utashirikiana na Raila Odinga katika uchaguzi mikuu wa Agosti 9.