Wachuuzi wa ngono wadinda kuwahudumia wanabodaboda

Muhtasari

• Baadhi ya wachuuzi wa ngono katika kaunti ya Mombasa wamesitisha huduma zaa kwa waendesha bodaboda kufuatia kisa cha wenzao kumshambulia mwanamke katika barabara ya Wangari Maathai.

• “Hawa watu ni wateja wangu ila kutoka leo, ila kwa wiki moja kutoka sasa hawatapata nafasi ya kuonja raha,” alisema.

Makahaba (Picha; Maktaba)
Makahaba (Picha; Maktaba)

Baadhi ya wachuuzi wa ngono katika kaunti ya Mombasa wamesitisha huduma zao kwa waendesha bodaboda kufuatia kisa cha wenzao kumshambulia mwanamke katika barabara ya Wangari Maathai.

Kama ishara ya kusimama na wakenya wengine kukemea kitendo hicho, ‘Aisha’ ambaye sio jina lake rasmi alisema kwamba wanabodaboda hawatafaidi huduma zake kwa wiki moja.

“Hawa watu ni wateja wangu ila kutoka leo, wiki moja kutoka sasa hawatapata nafasi ya kuonja raha,” alisema.

'Aisha’ anasema hatua hiyo ni njia moja ya kudai haki kwa wanawake wote wanaonyanyaswa na kudhalilishwa mbele ya umma.

“Hi ndo sehemu inayonipa chakula cha kila siku, lakini nipo tayari kulala njaa ndiposa vitendo vya aina hii vikomeshwe,” aliongezea.

Tayari serikali kupitia kwa rais Uhuru Kenyatta ilitangaza kuwa wahudumu wote wa bodaboda watapigwa msasa na kusajiliwa upya ili kulainisha sekta hiyo.