Ufisadi KEMSA kondomu na vyandarua vya mbu vikipotea

Muhtasari

• Mamlaka ya ugavi wa dawa za serikali ya KEMSA imejipata tena pabaya baada ya habari kutokea kwamba kondoni na vyandarua vya kujikinga dhidi ya mbu vyenye thamani zaidi ya milioni kumi na moja kutoweka katika maghala ya bodi hiyo.

Getty Images
Getty Images
Image: BBC Swahili

Mamlaka ya ugavi wa dawa za serikali ya KEMSA imejipata tena pabaya baada ya habari kutokea kwamba kondoni na vyandarua vya kujikinga dhidi ya mbu vyenye thamani zaidi ya milioni kumi na moja kutoweka katika maghala ya bodi hiyo.

Dawa zilizopotea zinaaminika kuibiwa na kuuzwa tena kimagendo kwa njia halali kwa wamiliki wa hospitali za kibinafsi na kemisti, kulingana na ripoti kutoka kwa shirika la Global Fund.

Bodi ya KEMSA inatuhumiwa kuongeza na kupaisha bei za dawa mara dufu ambapo inasemekana dawa zingine zimeongezwa bei kwa zaidi ya mara mia moja juu ya bei za kawaida na ambazo ni halisi kwa dawa hizo katika mataifa mengi.

Sasa inasubiriwa Shirika hilo la serikali kutoa taarifa kuhusu ufisadi huu ambao umegonga vichwa vya habari ikizingatiwqa ni chini ya miaka miwili, ambapo pia majipu ya ufisadi katika taasisi hiyo yalitumbuliwa na runinga moja nchini kwa kubatiliza fedha na vifaa vya kupambana na Corona.

Mfuko wa imataifa unafadhili mapambano ya Kenya dhidi ya virusi vya ukimwi, kifua kikuu, malaria na TB.

Zabuni ya thamani ya dola milioni 78 zilisemekana kupewa watu walio na ushawishi wa kisiasa na wafanyabiashara mwaka wa 2020 ambazo zilipotea pamoja na vifaa vya PPE vya madaktari waliokuwa wakishughulikia dharura ya Corona.

Tukio hilo lilimfanya Rais Uhuru Kenyatta kuvunja bodi yake na usimamizi wake mkuu.

Global Fund, ambayo imetoa zaidi ya milioni 160 kwa Kenya katika miongo miwili iliyopita, imependekeza uchunguzi zaidi wa Kemsa kuhusu dawa zilizopotea